Swali: Mwanamke akipata hedhi, au akisafika, baada ya kuwa amewahi wakati wa swalah wa kiwango cha Rak´ah moja. Je, analazimika kuilipa swalah hiyo?
Jibu: Mwanamke akipata hedhi baada ya kuingia wakati wa swalah, basi anawajibika kuikidhi swalah hiyo pale ataposafika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya swalah basi ameiwahi swalah.”[1]
Kwa hivyo mwanamke akiwahi muda wa swalah wa kiwango cha kuwahi Rak´ah moja kisha akapata hedhi kabla ya kuiswali, basi analazimika kuikidhi pale ataposafika.
Vivyo hivyo akisafika na hedhi kabla ya kumalizika wakati wa hedhi, basi anawajibika kuilipa swalah hiyo. Kwa mfano atasafika kwa kiwango cha Rak´ah moja kabla ya kuchomoza kwa jua, basi atawajibika kulipa swalah ya Fajr. Endapo atasafika kwa kiwango cha Rak´ah moja kabla ya kuzama kwa jua, basi atawajibika kulipa swalah ya ´Aswr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya ´Aswr kabla ya kuzama kwa jua, basi ameiwahi ´Aswr.”[2]
[1] Muslim (608).
[2] al-Bukhaariy (579) na Muslim (608).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/218)
- Imechapishwa: 27/04/2026
Swali: Mwanamke akipata hedhi, au akisafika, baada ya kuwa amewahi wakati wa swalah wa kiwango cha Rak´ah moja. Je, analazimika kuilipa swalah hiyo?
Jibu: Mwanamke akipata hedhi baada ya kuingia wakati wa swalah, basi anawajibika kuikidhi swalah hiyo pale ataposafika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya swalah basi ameiwahi swalah.”[1]
Kwa hivyo mwanamke akiwahi muda wa swalah wa kiwango cha kuwahi Rak´ah moja kisha akapata hedhi kabla ya kuiswali, basi analazimika kuikidhi pale ataposafika.
Vivyo hivyo akisafika na hedhi kabla ya kumalizika wakati wa hedhi, basi anawajibika kuilipa swalah hiyo. Kwa mfano atasafika kwa kiwango cha Rak´ah moja kabla ya kuchomoza kwa jua, basi atawajibika kulipa swalah ya Fajr. Endapo atasafika kwa kiwango cha Rak´ah moja kabla ya kuzama kwa jua, basi atawajibika kulipa swalah ya ´Aswr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya ´Aswr kabla ya kuzama kwa jua, basi ameiwahi ´Aswr.”[2]
[1] Muslim (608).
[2] al-Bukhaariy (579) na Muslim (608).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/218)
Imechapishwa: 27/04/2026
https://firqatunnajia.com/kupata-hedhi-kiwango-cha-kuwahi-rakah-moja-kabla-ya-kumalizika-kwa-wakati-wa-swalah/