Wakati ambapo kuna matarajio makubwa ya kuitikiwa du´aa siku ya ijumaa

Swali: Saa ya kuitikiwa du´aa ni pale imamu anapopanda mimbari?

Jibu: Hadiyth juu ya mada hii zitakuja katika somo la mwisho – Allaah akitaka. Pale imamu anapoketi juu ya mimbari ni wakati wa kuitikiwa. Akiomba du´aa ndani ya swalah yake au baina ya Khutbah mbili ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa du´aa. Vivyo hivyo baada ya alasiri mpaka wakati wa kuzama kwa jua kwa ambaye atakaa akisubiri swalah ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa du´aa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22600/متى-ساعة-الاستجابة-في-يوم-الجمعة
  • Imechapishwa: 08/07/2023