Swali: Nimepewa mtihani wa watoto wa ami yangu wasioswali. Je, inafaa kwangu kuwasalimia au kula nao?
Jibu: Muda wa kuwa hawaswali na swalah ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu… isitoshe Allaah (Ta´ala) amesema:
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ
“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake.” (58:22)
Kuna kupinga kupi kukubwa kuliko kutangaza kwa mtu kuacha swalah? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Baina ya mtu na kufuru au shirki ni kuacha swalah.”
´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Hana funga katika Uislamu kwa mwenye kuacha swalah.”
Allaah (Ta´ala) amesema katika Suurah al-Mudaththir:
مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ
“[Watawauliza]: “Nini kilichokuingizeni katika [Moto wa] Saqar?” Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.” (74:42-43)
Wasuse.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Khaatam-ul-Mursaliyn https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-10/lqa-mftoh-godian.mp3
- Imechapishwa: 17/10/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket