Wajinga kuhusu kumpa talaka mjamzito

Swali: Mara nyingi tunasikia kuwa mjamzito hana talaka. Je, hili ni sahihi au si sahihi?

Jibu: Haya ni maneno ya watu wa kawaida, ni maneno batili. Mjamzito talaka yake ni yenye kusihi. Anayo talaka. Kilichokataliwa ni kumtaliki mwanamke aliye ndani ya hedhi, aliye na damu ya uzazi au kumtaliki yule aliyefanya naye jimaa katika ndani ya kufika kwake. Hiki ndicho kisichojuzu kutalikiwa ndani yake. Ama mjamzito, basi talaka yake ni ya Kishari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Ibn ´Umar:

”… kisha amtaliki akiwa katika twahara au akiwa mjamzito.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1285/حكم-طلاق-المراة-حال-حملها
  • Imechapishwa: 19/06/2026