Mume ameonekana baada ya kipindi kirefu baada ya mke wake kuolewa

Swali: Tumesikia katika muhadhara kwamba mwanamke ana haki ya kuolewa baada ya kupita miaka minne tangu kupotea kwa mume wake. Ni ipi hukumu ikiwa mume wake wa kwanza akarudi? Je, abakie na wa pili au amrudie wa kwanza? Akimrudia wa kwanza itakuwaje?

Jibu: Mtu akipotea miongoni mwa jamaa zake na hajulikani yuko wapi, basi mara nyingi ni kwamba amekufa. Akipotea miongoni mwa watu katika miji na vijiji vyao na haijulikani alikoenda, zikisha kupita miaka minne kama alivyoamua ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh), wanafarikishwa na mwanamke aamrishwe aingie katika eda, kisha aolewe. Akionekana mume wake wa kwanza, watarejea mahakamani na mahakama ya Kishari´ah ndiyo itakayoangalia hukumu ya hali yao.

Mwanafunzi: Eda yake itakuwa miezi minne na siku kumi?

Ibn Baaz: Ni miezi minne na siku kumi, kama mtu aliyekufa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1284/حكم-من-تزوجت-بعد-فقد-زوجها-ثم-عاد-بعد-ذلك
  • Imechapishwa: 19/06/2026