Swali: Je, mwanaume amwache mkewe kwa sababu ya ombi la wazazi wake au mmoja wao licha ya kwamba maelewano baina ya wanandoa yapo?
Jibu: Maana hii imeshatangulia na kwamba wajibu ni kutatua tatizo kwa maneno mazuri pamoja na wazazi wake na pamoja naye. Amuhimize mkewe juu ya kuwa na mwenendo mwema pamoja nao na kuwafanyia upole. Vilevile azungumze na wazazi wake kwamba yeye ni mwanamke mwema na anayenifaa, basi ninawaomba muwe na msamaha na muache kudai tufarakane. Afanye awezalo ikiwa yeye ni mwema katika nafsi yake na hana shida. Lakini ikiwa madai ya wazazi wawili au mmoja wao yapo kwa sababu ya dosari ndani yake, kwa kuwa ameacha njia iliyonyooka, anatuhumiwa kwa uovu na dalili na sababu ziko wazi, hapo wajibu ni kuwatii katika hali hii.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1273/حكم-طلاق-الزوجة-مراعاة-لطلب-والد-الزوج
- Imechapishwa: 19/06/2026
Swali: Je, mwanaume amwache mkewe kwa sababu ya ombi la wazazi wake au mmoja wao licha ya kwamba maelewano baina ya wanandoa yapo?
Jibu: Maana hii imeshatangulia na kwamba wajibu ni kutatua tatizo kwa maneno mazuri pamoja na wazazi wake na pamoja naye. Amuhimize mkewe juu ya kuwa na mwenendo mwema pamoja nao na kuwafanyia upole. Vilevile azungumze na wazazi wake kwamba yeye ni mwanamke mwema na anayenifaa, basi ninawaomba muwe na msamaha na muache kudai tufarakane. Afanye awezalo ikiwa yeye ni mwema katika nafsi yake na hana shida. Lakini ikiwa madai ya wazazi wawili au mmoja wao yapo kwa sababu ya dosari ndani yake, kwa kuwa ameacha njia iliyonyooka, anatuhumiwa kwa uovu na dalili na sababu ziko wazi, hapo wajibu ni kuwatii katika hali hii.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1273/حكم-طلاق-الزوجة-مراعاة-لطلب-والد-الزوج
Imechapishwa: 19/06/2026
https://firqatunnajia.com/wazazi-wanamtaka-mwanao-amtaliki-mkewe/