Wajibu wa waislamu baada ya kitendo cha kigaidi ubelgiji

Swali: Ni wajibu gani walionao waislamu magharibini na khaswa baada ya yale yaliyotokea Ubelgiji?

Jibu: Ni wajibu kwa waislamu kumcha Allaah (´Azza wa Jall) popote walipo na wafanye kadri na wawezavyo kumtomdhuru yeyote.

Isitoshe waonyeshe waziwazi kujitenga kwao mbali na waharibifu Ubelgiji. Kitendo kile kimeharamishwa kwa mujibu wa Shari´ah. Anakuja muislamu na kuteketeza maisha ya watu ilihali hayuko vitani wala katika jihaad pamoja nao na kufikiria kuwa kitendo hicho kinapelekea kupata thawabu… bali kinasababisha dhambi mbele ya Allaah. Allaah ameamrisha kufanya wema juu ya kila kitu.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=885NvleOhDU
  • Imechapishwa: 29/11/2020