Swali: Una nasaha yoyote kwa mtu ambaye anawatukana wanachuoni ambao wamesimama kwa kazi ya kuwaraddi wenye kwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah?

Jibu: Ni juu yake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa sababu anachukia haki. Kuwaraddi watu wa batili ni haki. Kubainisha kosa la kielimu la mwenye kukosea ni jambo la haki na la wajibu kufanya. Huyu anataka elimu ifichwe. Ni juu yake kutubu na amuombe Allaah msamaha juu ya hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15208
  • Imechapishwa: 28/06/2020