Waislamu – maadui wa kufa wa Khawaarij  

Imesihi katika “al-Musnad” ya Imaam Ahmad kupitia kwa Abu Umaamah na Ibn Abiy Awfah kwa maana kama hiyo ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu Khawaarij:

“Bila ya shaka ni mijibwa ya Motoni.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza pia jinsi watakavyowaua waumini na kuwaacha makafiri. Ikawa hivyo. Wakati myahudi anapopita karibu yao wanasema “Mlinzi wa Mtume Muhammad” na wanamuacha anapita. Lakini wakati ‘Abdullaah bin Khabbaab bin al-Aratt alipowapitia, wakamuomba asimulie Hadiyth kutoka kwa baba yake. Akawaeleza kuhusu Hadiyth inayotahadharisha fitina na kumwaga damu na hapo wakawa wamemuua na kukata tumbo la mke wake alokuwa na mimba.

Wana mambo kama haya mengi. Ukisoma historia yao utaona jinsi kufanya vita wanavyowapiga vita Waislamu na kuwaacha makafiri na amani. Utaona jinsi walivo msaada mkubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu. Wakati mapigano ni makali zaidi kati ya Waislamu na makafiri Khawaarij wanajitokeza katika mji ili Waislamu walazimike kurudi ili waweze kulinda heshima zao dhidi ya Khawaarij.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 169
  • Imechapishwa: 26/08/2020