Waislamu kuwatumia makafiri kuwapiga vita makafiri wengine

Swali: Ni ipi dalili ya kujuzu kuomba msaada kutoka kwa kafiri juu ya kumpiga vita kafiri?

Jibu: Dalili zinaonesha kutojuzu kuomba msaada kutoka kwa kafiri. Haijuzu kuomba msaada kutoka kwa kafiri. Isipokuwa tu pale ambapo tutaogopa [sauti haiko wazi] na nguvu za makafiri. Katika hali hii ni sawa kuomba msaada wale ambao wanaweza kuzuia shari yao kutoka kwa watu wao. Hili linakuwa wakati wa dharurah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/hadist%20fitan-17-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015