Wafungaji wa mashambani walikuwa hawajui kuwa jimaa mchana wa Ramadhaan ni haramu

Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa hakimu X.

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Nakuwasilishia kisa cha bwana huyu X ambaye ametaja kwamba amemjamii mke wake mchana wa Ramadhaan hali ya kuwa walikuwa ni wajinga wakiishi mashambani na hawakuwa wakijua kuwa tendo la ndoa mchana wa Ramadhaan ni haramu. Likagueni jambo lao ikiwa ni wakweli na kwamba walikuwa hawajui kuwa ni haramu. Vinginevyo yatawagusa yale yanayopelekea katika kulipa na kutoa kafara kwa wote wawili muda wa kuwa mke naye alikubaliana na jambo hilo na watakamilisha yale mengine yanayopelekea kuhusiana na hilo.

Muftiy wa Saudi Arabia

14/03/1387

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/195-196)
  • Imechapishwa: 20/03/2024