Kuhusu hekima yake ni jambo liko wazi sana. Ndani yake kuna kuwatendea wema mafukara, kuwazuia kuwaomba watu katika masiku ya sikukuu ili washirikiane na matajiri katika furaha yao na iwe ni sikukuu ya wote. Ndani yake kuna kusifika na tabia ya ukarimu na kupenda kufariji. Ndani yake kumtakasa mfungaji kutokana na yale mapungufu, upuuzi na madhambi yanayopatikana kipindi cha funga yake. Ndani yake kuna kushukuru neema ya Allaah katika kukamilisha mfungo wa Ramadhaan, kusimama kuswali na kufanya ndani yake yale matendo mema yaliyowezekana. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr ili mfungaji atwaharishwe na mazungumzo ya upuuzi na uchafu ili kuwalisha masikini. Yule mwenye kuitoa kabla ya swalah basi ametoa zakaah yenye kukubaliwa na mwenye kuitoa baada ya swalah ametoa swadaqah miongoni mwa swadaqah.”

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Maajah[1].

Kuhusu aina ya wajibu katika kulisha ni kumpa chakula mwanadamu kama vile chakula, shayiri, mchele, zabibu, maziwa ya unga au vyakula vyenginevyo vinavyoliwa na watu. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea katika “as-Swahiyh” zao kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alifaradhisha kutoa pishi ya tende au pishi ya shayiri kuwa ni Zakaat-ul-Fitwr iliyowajibika kwa waislamu wote.”

Shayiri ilikuwa ni miongoni mwa vyakula vyao vinavyoliwa kipindi hicho, kama alivosema Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh):

“Tulikuwa wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tukitoa pishi ya chakula. Kipindi hicho chakula chetu kilikuwa ni shayiri, zabibu, maziwa ya unga na tende.”

Ameipokea al-Bukhaariy.

[1] Ameipokea pia ad-Daaqarutwniy na al-Haakim ambaye ameisahihisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 208-209
  • Imechapishwa: 20/03/2024