Swali: Je, yule mwenye kutaka kuwafunza watu mambo ya dini yao inatosheleza kuwa na shahada ya chuo kikuu au ni lazima awe na Tazkiyah ya wanachuoni?

Jibu: Ni lazima awe na elimu. Sio kila mwenye shahada anakuwa mwanachuoni. Ni lazima awe na elimu na uelewa katika dini ya Allaah. Shahada haitoi dalili ya elimu. Mtu anaweza kuwa na shahada na wakati huo huo ni katika wajinga kabisa wa kutupilia miongoni mwa watu. Upande mwingine mtu anaweza kuwa hana shahada yoyote lakini ni miongoni mwa wajuzi kabisa katika watu. Je, Shaykh Ibn Baaz ana shahada? Shaykh Ibn Ibraahiym ana shahada? Shaykh Ibn Humayd ana shahada? Je, watu hawa wana shahada? Pamoja na yote haya hawa ndio wanachuoni vigogo wa zama hizi. Kinachozingatiwa ni mtu kuwa na elimu na uelewa. Shahada haisemi kitu. Vielevile Tazkiyah hazisemi kitu. Haya hayazingatiwi.

Ukweli wa mambo humfichukua mtu. Wakati kunapotokea suala au janga ndio hubainika ni nani mwanachuoni na anayejifanya kuwa ni mwanachuoni na mjinga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-18.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020