Jinsi ya kutangamana na mwenye kuapa kwa kusema uongo

Swali: Tulisoma kwenye darsa ya Tawhiyd leo ya kwamba yule asiyeridhia anapoapiwa kwa jina la Allaah anakuwa sio mwenye kumuadhimisha Allaah. Je, inaingia katika hilo nikiapiwa na mtu na mimi najua kuwa ni muongo na hivyo nikawa sikukinaika wala kuridhia wala kukubali kiapo chake?

Jibu: Hichi ni kiapo cha uongo usikiridhie. Tunachomaanisha ni pale unapokuwa hujui. Katika hali hii mdhanie vyema [mwapaji]. Ikiwa hujui kuwa anasema uongo mdhanie vizuri na umuadhimishe Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama ukijua kuwa ni mwongo, hiki sio kiapo. Huu ni uongo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-18.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020