Kuongeza juu ya Adhkaar za asubuhi na jioni

Swali: Kuna mtu anataka kuongeza Adhkaar kutoka kwake katika Adhkaar za asubuhi na jioni.

Jibu: Midhali haziendi kinyume na Adhkaar zilizothibiti katika Qur-aan na Sunnah, ni sawa. Kukithirisha Adhkaar na du´aa ni sawa kwa sharti mtu asileti kitu kinachoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Iwe ni Adhkaar zenye kuafikiana na Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (51) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-11.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020