Swali: Je, imeshurutishwa kuwa na twahara wakati wa kuswalia jeneza?

Jibu: Ndio. Miongoni mwa masharti ya kusihi swalah ya jeneza ni kuwa na twahara. Mtu amtawadhishe maiti anayeswaliwa na mswalaji naye pia atawadhe. Hili ni lazima kwa kuwa ni swalah. Miongoni mwa masharti ya kusihi kwa swalah ni twahara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (51) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-11.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020