Kumjamii mke ndani ya eda ndio kumrejea     

Swali: Mtu akimtaliki mkewe na ndani ya eda akamwingilia pasi na kukusudia kwa kufanya hivo kumrejea. Lengo lake tu ilikuwa ni kukidhi haja yake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Huku kunahesabika ni kumrejea. Jimaa inahesabika ni kumrejea. Amemrudi kwa kufanya hivo. Jimaa ina nafasi kubwa kuliko kutamka tu “nimekurejea”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-10-18.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020