Tumeshatangulia katika kuifafanua Hadiyth hii ya kwamba miongoni mwa hayo – mtu kutorudi katika jambo aliloliacha kwa ajili ya Allaah – kunaingia pia yale yanayofanywa na baadhi ya watu kwa kujinasua na TV. Walipoona madhara na uharibifu wake hatimaye wakaamua kuiacha kwa ajili ya Allaah. Wakaivunja. Halafu wanakuja kuuliza kama wanaweza kuirudisha tena? Tunawaambia msiirudishe tena. Maadamu mmejinasua nayo kwa kutarajia thawabu kwa kuona uso wa Allaah, basi msirejee katika kitu mlichokiacha kwa ajili ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/58)
  • Imechapishwa: 25/01/2023