Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أبي هريرة عبد الرحمن بت صخر – رضي الله عنه – قال: قال رسول الله صلي الله عليه وسلم: ((إن الله لا ينظر إلي أجسادكم ولا إلي صوركم ولكن ينظر إلي قلوبكم)) . (رواه مسلم))

07 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ya Allaah hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu. Lakini anachotazama ni nyoyo zenu.”

Hadiyth hii inafahamisha yale yanayofahamishwa na maneno ya Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamme na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye kumcha Allaah zaidi kati yenu.”[1]

Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) hatazami viwiliwili vya viumbe: ni vikubwa au ni vidogo, ni mzima au ni mgonjwa. Kadhalika hatazami sura: ni mzuri au ni mbaya. Yote haya hayana maana yoyote mbele ya Allaah. Vivyo hivyo hatazami nasaba ya mtu: ana nasaba tukufu au duni. Hatazami mali na wala hatazami chochote katika haya. Hakuna baina ya Allaah na baina ya viumbe Vyake mafungamano yoyote isipokuwa kumcha. Yule anayemcha Allaah zaidi ndio ambaye anakuwa karibu zaidi na Allaah na mtukufu zaidi mbele ya Allaah.

Kwa hivyo, usijifakhari kwa mali yako, uzuri wako, mwili wako, watoto wako, ufupi wako, gari yako na mengineyo katika mambo haya ya kidunia. Kamwe! Allaah akikujaalia kumcha, basi hii ni fadhilah ya Allaah kwako. Mshukuru Allaah kwa hilo.

[1] 49:13

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/60-61)
  • Imechapishwa: 25/01/2023