Vitunguu na vitunguu saumu katika mikusanyiko ya watu

Swali: Je, makatazo ya kula vitunguu na vitunguu saumu ni maalum msikitini au kunaingia pia kuhudhuria swalah ya mkusanyiko kwa anayeswali nchikavu au safarini?

Jibu: Kila kulipo mkusanyiko wa watu haitakikani kwa mtu kuwaudhi hata kama sio msikitini. Akiwa katika mkusanyiko wa watu basi asiwaudhi. Ni haramu kuwaudhi waumini. Lakini msikitini ni kubaya zaidi. Kwa sababu ni kuwaudhi Malaika na wanadamu. Mbali na msikitini anawaudhi wanadamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 27/08/2021