Swali: Wale wataopewa madaftari yao kwa mkono wa kushoto inawahusu makafiri au ndani yake kunaingia pia waislamu wenye dhambi kubwa?

Jibu: Hili linawahusu makafiri. Kuhusu muislamu, hata kama atakuwa na dhambi kubwa ilio chini ya shirki, ni muislamu. Atapewa daftari lake kwa mkono wa kulia.

Kuna mapote potofu wanakata mkono wa kushoto wa maiti ili [siku atapofufuliwa] asiwe na mkono wa kushoto na hivyo apewe daftari kwa mkono wa kulia. Wanamfanya Allaah (Subhanaahu wa ´Alaa) kutokuwa muweza! Kana kwamba hawaamini kuwa Allaah (Ta´ala) atauumba mwili wote ukiwa mzima na kurudisha mkono wa kushoto na kufufuliwa hali ya kuwa ni mkamilifu. Hivi ni vituko kwa watu hawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-11-7.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020