Swali: Kuna mwanamke ana vito vyenye picha ya wanyama. Je, inafaa kuswali navyo?
Jibu: Haijuzu kuvaa vito vilivyo na picha ya wanyama au ya watu, si wakati wa kuswali wala nyakati zingine. Kwa sababu ni picha za kinyago. Ni haramu kubakiza vinyago na kuvitumia. Malaika hawaingii nyumba iliyo na picha. Yule ambaye yuko na vito hivi ni lazima kwake kwenda kwa sonara ili aondoshe vichwa vya wanyama hawa. Wakati kichwa kinapoondoshwa, basi uharamu unaondoka. Haijuzu kwake kubakiza vito hivi isipokuwa baada ya kuondoshwa vichwa vyake au kuvifuta mpaka kusibainike tena kuwa ni kichwa.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/361)
- Imechapishwa: 24/04/2026
Swali: Kuna mwanamke ana vito vyenye picha ya wanyama. Je, inafaa kuswali navyo?
Jibu: Haijuzu kuvaa vito vilivyo na picha ya wanyama au ya watu, si wakati wa kuswali wala nyakati zingine. Kwa sababu ni picha za kinyago. Ni haramu kubakiza vinyago na kuvitumia. Malaika hawaingii nyumba iliyo na picha. Yule ambaye yuko na vito hivi ni lazima kwake kwenda kwa sonara ili aondoshe vichwa vya wanyama hawa. Wakati kichwa kinapoondoshwa, basi uharamu unaondoka. Haijuzu kwake kubakiza vito hivi isipokuwa baada ya kuondoshwa vichwa vyake au kuvifuta mpaka kusibainike tena kuwa ni kichwa.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/361)
Imechapishwa: 24/04/2026
https://firqatunnajia.com/vito-vyenye-picha-za-wanyama/