Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na nguo za kulalia na kuhudhuria nazo msikitini?

Jibu: Hapana vibaya kuswali na nguo za kulalia muda wa kuwa ni safi, ni mamoja mtu amekuja nazo msikitini au mtu hakuja nazo. Isipokuwa ikiwa nguo hizo zinafanya watu kumkodolea macho kwa namna ya kwamba akasimangwa na akafanywa kuwa gumzo kwa watu. Katika hali hiyo mtu anatakiwa kuepuka kila kitu ambacho kinasababisha kusengenywa.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/362)
  • Imechapishwa: 24/04/2026