Mswaliji amekata nia ya swalah yake

Swali: Ni ipi hukumu mtu akikata nia katikati ya swalah?

Jibu: Akikata nia wakati yuko anaswali, basi inaharibika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”[1]

Huyu amenuia kukata, hivyo swalah yake inaharibika.

[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/449)
  • Imechapishwa: 24/04/2026