Nifungue mlango au nisifungue?

Swali: Mswaliji anasikia mtu anabisha hodi na hivyo akaanza kusita kama akate swalah yake au asikate. Je, swalah yake inaharibika?

Jibu: Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa swalah yake inaharibika ingawa hatoazimia kuikata. Wanazuoni wengine wakasema kuwa swalah haiharibiki kwa kusita. Msingi ni kubakia kwa nia na kusita hakuiharibu. Maoni haya ndio sahihi. Muda wa kuwa hakuazimia kuikata, basi anazingatiwa bado yuko ndani ya swalah.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/449)
  • Imechapishwa: 24/04/2026