Swali: Ni sahihi kwamba mwanamke analazimika kubadilisha nguo yake ya ndani wakati wa kila swalah?
Jibu: Sio sahihi. Muda wa kuwa nguo yake ya ndani ni safi, inafaa kwake kuswali nayo. Kunamsitiri zaidi kuliko kuswali bila kuivaa. Ikiwa nguo yake ya ndani ni najisi, basi analazimika kuivua na kuiosha. Ikishasafika basi ni sawa akaswali nayo.
Hapa kuna suala ambalo nataka kulizindua: baadhi ya watu wanakidhi haja kabla ya wakati wa swalah halafu wanatamba kwa maji, unapoingia wakati wa swalah wanaona kuwa wanalazimika kutamba tena hata kama hawakutekeleza haja. Lakini hilo si sahihi. Mtu akitekeleza haja ndogo au haja kubwa kisha akajisafisha na kutamba inavyotakiwa, halazimiki kutamba kwa mara nyingine. Bali inatosha kutawadha hata kama ametamba baadaye baada ya masaa mawili au matatu. Kutawadha ni kule kuosha uso na mikono, kupangusa kichwa na kuosha miguu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/385-386)
- Imechapishwa: 24/04/2026
Swali: Ni sahihi kwamba mwanamke analazimika kubadilisha nguo yake ya ndani wakati wa kila swalah?
Jibu: Sio sahihi. Muda wa kuwa nguo yake ya ndani ni safi, inafaa kwake kuswali nayo. Kunamsitiri zaidi kuliko kuswali bila kuivaa. Ikiwa nguo yake ya ndani ni najisi, basi analazimika kuivua na kuiosha. Ikishasafika basi ni sawa akaswali nayo.
Hapa kuna suala ambalo nataka kulizindua: baadhi ya watu wanakidhi haja kabla ya wakati wa swalah halafu wanatamba kwa maji, unapoingia wakati wa swalah wanaona kuwa wanalazimika kutamba tena hata kama hawakutekeleza haja. Lakini hilo si sahihi. Mtu akitekeleza haja ndogo au haja kubwa kisha akajisafisha na kutamba inavyotakiwa, halazimiki kutamba kwa mara nyingine. Bali inatosha kutawadha hata kama ametamba baadaye baada ya masaa mawili au matatu. Kutawadha ni kule kuosha uso na mikono, kupangusa kichwa na kuosha miguu.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/385-386)
Imechapishwa: 24/04/2026
https://firqatunnajia.com/mwanamke-anabadilisha-nguo-yake-ya-ndani-wakati-wa-kila-swalah/