Swali: Kuna mwanamke aliswali kinyume na Qiblah na baada ya kupita muda fulani ikambainikia kuwa ameswali kinyume na Qiblah. Je, swalah yake ni sahihi?
Jibu: Mtu akiswali kinyume Qiblah hali ya kufikiria kuwa ndipo kilipo Qiblah, ikiwa ni ndani ya mji basi analazimika kuirudia swalah yake. Kwa sababu anaweza kuwauliza wakazi wa nyumba au kutafuta msikiti ili kuweza kutambua ni wapi kipo Qiblah chake. Na kama yuko safarini na amejitahidi kufanya akiwezacho ili kuweza kuswali upande usahihi na hakuna mtu awezaye kumuuliza, halazimika kuirudia swalah yake.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/416)
- Imechapishwa: 24/04/2026
Swali: Kuna mwanamke aliswali kinyume na Qiblah na baada ya kupita muda fulani ikambainikia kuwa ameswali kinyume na Qiblah. Je, swalah yake ni sahihi?
Jibu: Mtu akiswali kinyume Qiblah hali ya kufikiria kuwa ndipo kilipo Qiblah, ikiwa ni ndani ya mji basi analazimika kuirudia swalah yake. Kwa sababu anaweza kuwauliza wakazi wa nyumba au kutafuta msikiti ili kuweza kutambua ni wapi kipo Qiblah chake. Na kama yuko safarini na amejitahidi kufanya akiwezacho ili kuweza kuswali upande usahihi na hakuna mtu awezaye kumuuliza, halazimika kuirudia swalah yake.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/416)
Imechapishwa: 24/04/2026
https://firqatunnajia.com/mwanamke-ameswali-kinyume-na-qiblah/