Swali: Vipi Allaah anathibitishiwa sifa ya istihzai pale aliposema:

اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ

“Allaah anawadhihaki wao.”[1]?

Jibu: Anawafanyia ishtihzai na kuwafanyia njama kama wao walivofanya. Ni vitimbi vya haki na istihzai ya haki. Allaah (Ta´ala) anasifiwa kwa sifa hiyo. Kinachosemwa vibaya ni kufanya istihzai kwa batili na kufanya vitimbi kwa batili. Lakini kuwafanyia istihzai ni kwa mukabala wa istihzai yao. Wakati walipofanya istihzai ndipo Naye akawafanyia istihzai, vitimbi, njama na hadaa. Ni sifa za haki ambazo anasifiwa nazo kwa njia inayolingana na Allaah (Jalla wa ´Alaa).

[1] 02:15

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 106-107
  • Imechapishwa: 09/02/2023