Swali: Sifa ya maneno ya Allaah ni ya kidhati au ya kimatendo?

Jibu: Msingi wake ni ya kidhati. Inafaa kusema kwamba ni sifa ya kidhati na inafaa pia kusema kwamba ni ya kimatendo. Anaifanya pale anapotaka na hivyo ni ya kidhati na pia inaitwa kuwa ni ya kimatendo kwa sababu inatokea kwa mujibu wa matashi Yake. Anazungumza kwa dhati Yake (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 107
  • Imechapishwa: 09/02/2023