Vitasa na kalamu za dhahabu na fedha feki

Swali: Hii leo kunauzwa kalamu zenye ncha ya dhahabu au vitasa vya milango vyenye dhahabu feki na si dhahabu halisi?

Jibu: Salama zaidi ni kuviepuka. Pengine mtu akasema kuwa baadhi ya wanazuoni, kama vile Shaykh Taqiyy-ud-Diyn (Rahimahu Allaah) na wengineo, wanaona kuwa kitu kidogo kinasamehewa. Lakini tahadhari zaidi ni kuviepuka ili kufunga mlango wa kuchukulia wepesi. Mtu akichukua tahadhari katika jambo hili ndio bora zaidi.

Swali: Vipi kalamu za fedha?

Jibu: Kalamu za fedha ni jambo jepesi kidogo. Lakini vyema zaidi akiviepuka vyote hivyo, ingawa vitu vya dhahabu ndio vibaya zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24705/حكم-استعمال-ما-كان-مموها-بذهب-او-فضة
  • Imechapishwa: 29/11/2024