Ibn Baaz kuhusu kuanza kumtaja Allaah chooni kabla ya kutawadha

Swali: Je, baadhi ya nyakati aseme “Bismillaah” akiwa ndani ya choo?

Jibu: Akihitajia kutawadha ndani ya choo, kwa sababu baadhi ya maduka sehemu za kunawia zipo ndani [ya vyoo], basi aseme “Bismillaah” ndani yake. Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa ni wajibu kusema hivo. Jambo la wajibu linaondosha kitu kilichochukizwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24708/حكم-التسمية-في-دورة-المياه-عند-الوضوء
  • Imechapishwa: 29/11/2024