Muislamu kunywa masalia ya maji ya makafiri

Swali: Vipi kuhusu kunywa masalia ya makafiri?

Jibu: Halidhuru, kama vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyotawadha kwa maji kutoka kwenye kiriba cha mwanamke mshirikina. Haidhuru ukinywa kutoka kwenye maji walionayo muda wa kuwa hujui kutoka kwao isipokuwa kheri tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24706/هل-يجوز-شرب-سور-الكافر
  • Imechapishwa: 29/11/2024