Vitabu na kanda za waliokuwa Salafiyyuun kisha baadaye wakapinda

Swali: Inafaa kwetu kusikiliza kanda na kusoma vitabu vya zamani vya wale ambao walikuwa wakifuata mfumo sahihi kisha baadaye wakapinda?

Jibu: Mimi sipendekezi kusoma vitabu vyao wala kusikiliza kanda zao. Napendekezwa na maneno matukufu yaliyosemwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) pale aliposema:

“Lau Allaah asingefanya kupatikana kwa al-Bukhaariy na Muslim basi dini yake isingelipotea.”

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi Tumeteremsha Ukumbusho huu na hakika Sisi bila shaka ndio Tutakaouhifadhi.” (15:09)

Kwa hivyo nawashauri kujitenga mbali na vitabu vyao, kanda zao na kuhudhuria mihadhara yao. Wao ndio wanahitajia ulinganizi, kurejea katika Qur-aan na Sunnah na watubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kutokana na yale yaliyotokea kwao juu ya suala la Ghuba na kwenginepo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 209