Mchinjaji ndiye hafai kukata nywele na kucha zake na si wale wachinjiwa

Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zitapoingia zile siku kumi [za Dhul-Hijjah] na akataka mmoja wenu kuchinja, basi asichukue/asikate kutoka katika nywele wala kucha zake chochote mpaka achinje kwanza.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… wala ngozi yake.”

Hiyo ina maana kwamba ni haramu mpaka zije dalili zinazogeuka kutoka katika uharamu huo.

Kutokana na haya haifai kwa yule ambaye amekusudia kuchinja kukata chochote kutoka katika ngozi yake, nywele zake wala kucha zake baada ya kuingia Dhul-Hijjah. Makatazo haya yanaendelea mpaka pale atapochinja. Makatazo haya yanamgusa mchinjaji na sio wale wanaochinjiwa. Kwa hivyo sio haramu kwa familia kufanya hayo yaliyotajwa. Wao hawachinji isipokuwa tu wanachinjiwa.

[1]Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ibnothaimeen.com/all/noor/article_6303.shtml
  • Imechapishwa: 12/07/2020