Vita Syria – pasina manufaa, umgwagikaji wa damu na uharibifu

Swali: Kuna propaganda kati ya vijana ambao wanaita katika Jihaad Syria. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Jihaad ina vidhibiti na masharti yake. Yametajwa katika vitabu vya ´Aqiydah. Sijisemei kutoka kwangu mwenyewe. Yametajwa katika vitabu vya ´Aqiydah vya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa ni ncha ya mkuki wa Uislamu. Jihaad ni muhimu. Hata hivyo ni lazima Jihaad iwe katika sifa ambayo imeweka Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Lakini vita vikiwa pasina ya kanuni za Kishari´ah na udhibiti uliyowekwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), inakuwa shari, umwagikaji wa damu na uharibifu. Halileti manufaa yoyote. Halileti manufaa yoyote. Ni lazima kuwepo vidhibiti.

Kidhibiti muhimu zaidi ni Jihaad iwe chini ya uongozi wa mtawala wa Kiislamu. Mtawala au naibu wa mtawala ambaye atawaongoza Waislamu. Hivyo ndivyo ilikuwa kwa Salaf-us-Swaalih. Inapokuja katika Jihaad walikuwa wakirejea kwa watawala. Watawala ndio waliokuwa wakipanga hilo na wakilisimamia. Hii ndio Jihaad katika njia ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-01-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 23/04/2015