Swali: Baadhi ya waandishi wanaadika kisa na kusema kuwa ni kwa njia ya mawazo tu.

Jibu: Haitakikani kufanya hivo. Inazingatiwa ni katika uwongo. Haitakikani kwa mtu kuandika kitu isipokuwa cha ukweli tu na chenye kuwafaidisha watu. Nasaha zilizonakiliwa na wanazuoni zinatosha kuwa na faida na manufaa. Ama kusema uwongo na kuandika vitu vya mawazo kutoka katika fikira zake ni uwongo na haitakikani. Nachelea kuwa jambo hilo linakusanywa na dhambi ya uwongo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23391/حكم-قول-بعض-الكتاب-هذا-من-نسج-الخيال
  • Imechapishwa: 11/01/2024