Vipi Saudi Arabia ni nchi ya Kiislamu na kumejaa maasi?

Ama kupatikana maasi na makosa – yaani Saudi Arabia – haya ndio maumbile ya binaadamu wote tokea wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makhaliyfah wake waongofu. Watu walikuwa wakifanya makosa na maasi. Vivyo hivyo masiku ya nchi zingine za Kiislamu baada yao. Hakuna aibu kwa kupatikana maasi lakini aibu inakuja pale ambapo wale wenye kuyatenda watakuwa hawaadhibiwi ikiwa maasi hayo yanapelekea mwenye nayo kusimamishiwa adhabu.

Kuhusiana na kuwanasihi viongozi na watawala ni jambo la wajibu kwa wanachuoni wa Ummah. Katika “as-Swahiyh” ya Muslim imepokelewa:

“Dini ni kupeana nasaha” alisema hivyo mara tatu.” Tukasema: “Kwa nani, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni kwa Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, waislamu wa kawaida na viongozi wao.” Muslim (95).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bid´ah – Dhwawaabitwuhaa wa atharuhaa as-Sayyiu´ fiyl-Ummah, uk. 42
  • Imechapishwa: 27/08/2020