Vipi Mtume aliwaona watu wa Motoni na Qiyaamah bado?

Swali: Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba usiku alipopandishwa [mbinguni] aliona baadhi ya watu Motoni ambao wamefanya madhambi. Vipi hilo na wakati Qiyaamah bado hakijasimama na siku ya hesabu haijafika?

Jibu: Hili ni haki. Ni wajibu kuliamini. Haijuzu kuingia katika mambo ambayo ni kazi ya kipekee ya Allaah (Ta´ala).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/269)
  • Imechapishwa: 23/08/2020