Mtume (´alayhis-Salaam) anasahau?

Swali: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasahau au hasahau?

Jibu: Ndio, inajuzu kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusahau. Lakini hakubaliwi katika mambo yanayohusiana na Shari´ah, bali Allaah humfunza. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi ni mwanadamu, ninasahau kama mnavyosahau. Hivyo basi nikisahau nikumbusheni.”

Ilikuwa wakati aliposahau katika swalah ya ´Aswr.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/270)
  • Imechapishwa: 23/08/2020