Mtume alipandishwa mmbinguni kwa roho bila ya mwili ay vyote viwili?

Swali: Kusafirishwa usiku kwa kupandishwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka msikiti wa al-Aqswaa na kwenda mbinguni ilikuwa ni kwa roho na mwili vikiwa pamoja au ilikuwa ni roho peke yake na ni ipi dalili

Jibu: Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanasema kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisafirishwa usiku kutoka msikiti Mtakatifu usiku na kupelekwa msikiti wa al-Aqswaa kwa roho na mwili wake. Amesema (Ta´ala):

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

”Utakasifu ni wa Ambaye alimsafirisha mja Wake usiku kutoka al-Masjid al-Haraam kwenda al-Masjid al-Aqswaa ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake ili tumuonyeshe baadhi ya ishara Zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima.” (17:01)

Neno “mja” limekusanya roho na kiwiliwili vyote pamoja. Kadhalika alisafirishwa kutoka msikiti wa al-Aqswaa na kupandishwa mbinguni (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) akiwa na roho na kiwiliwili. Hilo limethibiti kwa Hadiyth nyingi ambazo amezitaja Ibn Kathiyr na wengine wakati walipokuwa wanaifasiri Aayah hii.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/267)
  • Imechapishwa: 23/08/2020