Vipi kwa mtu ambaye amesitisha swawm ya kafara ya miezi miwili mfululizo kwa sababu ya udhuru?

Swali: Mtoto wangu alifariki na nikaamrishwa kufunga miezi miwili mfululizo. Nimefunga mwezi mmoja na siku tatu na zimebaki siku ishirini na saba. Kisha nikapata ujauzito na nikapata maradhi mengine na sikuweza kufunga baada ya hapo. Ni ipi hukumu?

Jibu: Ikiwa mtu analazimika kufunga miezi miwili mfululizo, kisha akapatwa na maradhi au mwanamke akapatwa na hedhi, basi anafungua kwa sababu ya maradhi au anafungua kwa sababu ya hedhi, kisha anakamilisha baada ya kuondoka maradhi au kuondoka hedhi, pale anapoweza kufunga. Anakamilisha swawm ambayo iko juu yake, kwa sababu maradhi ni udhuru na hedhi ni udhuru. Ikiwa mtu amepatwa na maradhi yaliyomzuia kufunga katika kufunga miezi miwili mfululizo, kama kafara ya kuua au kafara ya kumfananisha mke na mama au kafara ya kufanya tendo la jimaa katika Ramadhaan, basi anakamilisha baada ya kuondoka udhuru.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3505/حكم-من-عليه-صيام-كفارة-شهرين-متتابعين-وافطر-خلالهما-لعذر
  • Imechapishwa: 29/08/2026