Mjane amelazimika kufanya kazi katika kampuni yenye mchanganyiko

Swali: Kuna mwanamke amefiwa na mume wake na ameacha watoto na hakuna anayewagharamia. Ametoka kutafuta riziki kwa ajili ya watoto wake katika uwanja wa kazi baina ya wanaume na wanawake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni juu yake yake kutafuta kazi na kuwahudumia watoto wake, lakini kwa njia zilizo halali. Hapana vibaya kufanya kazi katika uwanja wa wanawake, si katika uwanja wa wanaume. Ama kuwa kati ya wanaume, hapana. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameweka katika yale aliyoruhusu yanayotosheleza badala ya yale aliyoharamisha. Kwa hiyo afanye kazi kama muuguzi kwa wanawake tu, afanye kazi katika nyumba iliyo salama kwa ujira unaojulikana, kazi ambazo anazifanya na mfano wa hayo katika njia zilizo salama zilizo mbali na khatari.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3493/عمل-المراة-للحاجة-في-وظيفة-مع-الاختلاط
  • Imechapishwa: 29/08/2026