Swali: Ni ipi hukumu ya vifaa vya kuchezea vya watoto ambavyo vina umbo la wanyama?
Jibu: Hili ndani yake kuna makinzano baina ya wanazuoni. Vifaa vya kuchezea vya watoto, miongoni mwao wapo waliojuzisha hilo na miongoni mwao wapo walioharamisha hilo. Lililo la tahadhari zaidi kwa muumini ni asichukue picha zinazojulikana zilizo na umbo kamili ambazo hutumiwa na watoto. Inafaa kwake asizichukue na awabadilishie vitu vya kawaida ambavyo watu walikuwa wakivifanya zamani, kama vijiti ambapo wanatia ndani yake kitu au mfano wa hivyo ambavyo havina umbo kamili linalofanana na picha ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amelaani mwenye kuzifanya. Kwa maana picha za kawaida ambazo hazina umbo kamili linaloingia katika Hadiyth, umbo kamili lenye kichwa, jicho, pua na mfano wa hayo. Hivi ndivyo waarabu wa zamani walivyokuwa wakifanya, wanachukua vijiti au mifupa ambapo wanavivalisha nguo na kuweka kijiti kingine kama mikono, hivi ni vitu visivyofanana na umbo kamili.
Ama picha zilizopo sasa ni wazi zinafanana na uumbaji wa Allaah. Kwa hiyo baadhi ya wanazuoni wamezuia hilo hata kwa watoto, na baadhi ya wanazuoni wameliruhusu hilo kwa watoto kwa sababu imethibiti kwamba ilikuwa kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) wanasesere na alikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akimkubalia.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3500/حكم-العاب-الاطفال-التي-على-شكل-حيوانات
- Imechapishwa: 29/08/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya vifaa vya kuchezea vya watoto ambavyo vina umbo la wanyama?
Jibu: Hili ndani yake kuna makinzano baina ya wanazuoni. Vifaa vya kuchezea vya watoto, miongoni mwao wapo waliojuzisha hilo na miongoni mwao wapo walioharamisha hilo. Lililo la tahadhari zaidi kwa muumini ni asichukue picha zinazojulikana zilizo na umbo kamili ambazo hutumiwa na watoto. Inafaa kwake asizichukue na awabadilishie vitu vya kawaida ambavyo watu walikuwa wakivifanya zamani, kama vijiti ambapo wanatia ndani yake kitu au mfano wa hivyo ambavyo havina umbo kamili linalofanana na picha ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amelaani mwenye kuzifanya. Kwa maana picha za kawaida ambazo hazina umbo kamili linaloingia katika Hadiyth, umbo kamili lenye kichwa, jicho, pua na mfano wa hayo. Hivi ndivyo waarabu wa zamani walivyokuwa wakifanya, wanachukua vijiti au mifupa ambapo wanavivalisha nguo na kuweka kijiti kingine kama mikono, hivi ni vitu visivyofanana na umbo kamili.
Ama picha zilizopo sasa ni wazi zinafanana na uumbaji wa Allaah. Kwa hiyo baadhi ya wanazuoni wamezuia hilo hata kwa watoto, na baadhi ya wanazuoni wameliruhusu hilo kwa watoto kwa sababu imethibiti kwamba ilikuwa kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) wanasesere na alikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akimkubalia.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3500/حكم-العاب-الاطفال-التي-على-شكل-حيوانات
Imechapishwa: 29/08/2026
https://firqatunnajia.com/salama-zaidi-ni-kuepuka-doli-za-watoto-za-umbo-la-wanyama-au-wanadamu/