Vipi kuhusu kumtekelezea adhabu kafiri anayefanya uhalifu katika nchi ya Kiislamu?

Swali: Shari´ah ya Kiislamu inafaa kwa kila zama na kila mahali. Ikiwa tutatekeleza Shari´ah katika nchi ambayo wengi wao ni waislamu na kuna idadi ya wafuasi wa Kitabu na wasio na dini kabisa, ni ipi hukumu ya kutekeleza Shari´ah juu yao? Ikiwa mfuasi wa Kitabu mwanamume au mwanamke atafanya uhalifu unaopelekea kutekelezewa adhabu ya kidini na yakapatikana masharti yote ya kusimamisha adhabu juu yake, je, huzuiwa kutekelezewa adhabu kwa sababu ya tofauti ya dini? Ni ipi hukumu ikiwa mtendaji wa uhalifu hana dini, kwa maana ni kafiri?

Jibu: Hili ni jambo lililofafanuliwa kwa wanazuoni na kubainishwa kwa wanazuoni. Ikiwa katika nchi kuna manaswara, mayahudi au watu wengine katika makafiri, basi ni juu yao kushikamana na mipaka ya Shari´ah. Ni juu ya dola kutekeleza kwao hukumu ya Allaah (´Azza wa Jall). Ikiwa wamelipa kodi na wakashikamana na hukumu za dola na hukumu za Uislamu, basi juu ya dola ni kuwalinda na dhuluma, isimuache yeyote awadhulumu, kuwapa haki za raia zinazofanana na wao na kusimamisha juu yao amri ya Allaah ikiwa wameenda kinyume na Shari´ah ya Allaah. Wasidhihirishe dini yao wala maovu yao mbele ya waislamu. Bali iwe ndani ya nyumba zao na ndani ya maeneo yao ili wasidhihirishe shari yao kwa waislamu na wala dini yao kwa waislamu.

Kwa kumalizia ni kwamba haya yana hukumu zake katika utawala wa Kiislamu. Ni lazima juu ya watawala kutekeleza hukumu za Kiislamu ambazo wamezitaja wanazuoni juu ya mayahudi, manaswara na juu ya waabudia moto, juu ya wabudha katika nchi zao na wengineo katika wale ambao Shari´ah imeruhusu kubaki kwao. Ama wale ambao Shari´ah haikuruhusu kubaki kwao, basi hawa wanashughulikiwa kwa kile kinachotakiwa na Shari´ah. Ikiwa Shari´ah inataka waondolewe, basi wanaondolewa. Ikiwa inataka wauawe, basi wanauawa. Ni lazima ihukumiwe kwao amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika yale yanayowalazimu. Aidha ni lazima kuwalinda na dhuluma na kuwapa haki zao ambazo zimekubaliwa juu yake masharti kati yao na mtawala. Ikiwa masharti yaliyopo kati yao na mtawala hayakutekelezwa, basi nao pia hawatekelezwi baadhi ya hukumu. Haya ni mambo ambayo hayakuachwa, bali yana hukumu zilizoelezwa katika mkataba na hukumu kuhusu makafiri waliopewa mkataba wa amani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3458/حكم-تطبيق-الشريعة-الاسلامية-على-الكفار-في-بلاد-المسلمين
  • Imechapishwa: 02/09/2026