Swali: Katika siku hizi kumetokea vazi kwa wanaume lenye sehemu ya hariri. Ni ipi hukumu ya kulivaa ikiwa kiwango cha hariri hii siyo feki?
Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
“Imehalalishwa dhahabu na hariri kwa wanawake wa ummah wangu na vimeharamishwa kwa wanaume wao.”
Kwa hiyo hariri ni haramu kwa wanaume na ni halali kwa wanawake. Isipokuwa sehemu ya vidole viwili, vitatu au vinne, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msivae hariri… ”
Anawaongelesha wanaume
“… isipokuwa sehemu ya vidole viwili, vitatu au vinne.”
Kama alivyosimulia ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) katika Swahiyh.
Kwa hiyo ikiwa kipande kilichopo katika vazi ni sehemu ya vidole viwili, vitatu au vinne, basi hakuna ubaya. Mfano kiraka katika vazi cha hariri, mfano vifungo, mfano alama ya hariri, alama katika vazi iliyowekwa katika vazi kama alama na mfano wa hayo, haya yanaruhusiwa. Makusudio ni kwamba kiasi cha vidole viwili, vitatu au vinne tu katika vazi. Kinachozidi juu ya hili katika mavazi ya mwanaume ni haramu kutokana na hariri.
Mwanafunzi: Inahusu ya kawaida na ya kutengenezwa?
Ibn Baaz: Makusudio ni hariri ile inayotokana na kitu kinachojulikana, kutoka kwa funza wa hariri.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3475/لبس-الحرير-للرجال-والقدر-الجاىز-في-ذلك
- Imechapishwa: 02/09/2026
Swali: Katika siku hizi kumetokea vazi kwa wanaume lenye sehemu ya hariri. Ni ipi hukumu ya kulivaa ikiwa kiwango cha hariri hii siyo feki?
Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
“Imehalalishwa dhahabu na hariri kwa wanawake wa ummah wangu na vimeharamishwa kwa wanaume wao.”
Kwa hiyo hariri ni haramu kwa wanaume na ni halali kwa wanawake. Isipokuwa sehemu ya vidole viwili, vitatu au vinne, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msivae hariri… ”
Anawaongelesha wanaume
“… isipokuwa sehemu ya vidole viwili, vitatu au vinne.”
Kama alivyosimulia ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) katika Swahiyh.
Kwa hiyo ikiwa kipande kilichopo katika vazi ni sehemu ya vidole viwili, vitatu au vinne, basi hakuna ubaya. Mfano kiraka katika vazi cha hariri, mfano vifungo, mfano alama ya hariri, alama katika vazi iliyowekwa katika vazi kama alama na mfano wa hayo, haya yanaruhusiwa. Makusudio ni kwamba kiasi cha vidole viwili, vitatu au vinne tu katika vazi. Kinachozidi juu ya hili katika mavazi ya mwanaume ni haramu kutokana na hariri.
Mwanafunzi: Inahusu ya kawaida na ya kutengenezwa?
Ibn Baaz: Makusudio ni hariri ile inayotokana na kitu kinachojulikana, kutoka kwa funza wa hariri.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3475/لبس-الحرير-للرجال-والقدر-الجاىز-في-ذلك
Imechapishwa: 02/09/2026
https://firqatunnajia.com/ni-haramu-kwa-wanaume-kuvaa-mavazi-ya-hariri/