Inapendekezwa kwa yule anayesoma Qur-aan na akapita kwenye Aayah ya rehema, basi amwombe Allaah (Ta´ala) katika fadhilah Zake, na anapopita kwenye Aayah ya adhabu, ajilinde kwa Allaah dhidi ya shari na adhabu au amwombe Allaah amsalimishe na amwombe amlinde na kila kinachochukiza na mfano wa hayo.
Anapopita kwenye Aayah ya kumtakasa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kutokana na mapungufu, basi aseme:
سبحانه و تعالى
”Ametakasika na ametukuka kutokana na mapungufu.”
تبارك و تعالى
”Amebarikika na ametukuka.”
جلت عظمة ربنا
”Umetukuka na umekuwa juu utukufu wa Mola wetu.”
Imethibiti kutoka kwa Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba amesema:
”Niliswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku mmoja. Akaanza kwa ”al-Baqarah” ambapo nikajiambia kwamba atarukuu kwenye Aayah ya mia moja, lakini akaendelea. Nikajiambia kwamba atasoma yote katika Rak´ah moja, akaendelea. Nikajiambia kwamba atarukuu baada yake. Kisha akaanza an-Nisaa’ na kuisoma yote. Kisha akaanza Aal ´Imraan na kuisoma yote. Alikuwa akisoma kwa utararibu na ipasavyo. Akipita katika Aayah yenye kumtakasa Allaah, basi anamtakasa Allaah, akipita kwenye Aayah ya kuomba anaomba na akipita kwenye Aayah ya kujilinda anaomba hifadhi.”[1]
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.
Wakati huo Suurah ”an-Nisaa’” ilikuwa kabla ya ”Aal ´Imraan”.
Maswahiba wetu (Rahimahum Allaah) wamesema kwamba inapendekezwa kwa kila msomaji wa Qur-aan kufanya maombi haya, kuomba hifadhi na kumtakasa Allaah na mapungufu, ni mamoja awe yuko ndani ya swalah au nje ya swalah. Vilevile wamesema kwamba inapendekezwa pia kwa mswaliji ambaye ni imamu, anayeswali peke yake na maamuma, kwa sababu hii ni du´aa na hivyo wote wanashirikiana katika hilo. Ni kama ilivyo kusema “Aamiyn” baada ya ”al-Faatihah”. Haya tuliyoyataja ya kupendekezwa kuomba na kujilinda ndiyo maoni ya ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) na kikosi kikubwa cha wanazuoni (Rahimahumu Allaah). Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) amesema kuwa haipendekezwi bali ni jambo linalochukiza ndani ya swalah. Sahihi ni maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni kutokana na yale tuliyoyatanguliza.
[1] Muslim (772).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 59
- Imechapishwa: 02/09/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 59
Imechapishwa: 02/09/2026
https://firqatunnajia.com/52-kuomba-duaa-wakati-wa-kisomo-cha-qur-aan/