Vipi ISIS wameshikamana na maneno ya Mtume?

Fitina imekuwa kubwa katika Ummah huu kwa sababu ya umwagikaji wa damu, ukatwaji wa vichwa, utundikwaji wa vichwa na kukithiri kwa ukatwaji wa viungo na ueneaji wa fitina ya upofu na kukutana kwa ajili ya kukuza ufisadi, Takfiyr, malipuaji yasiyokatika, uharibifu na madonda makubwa yanayoendelea hivi sasa kwa muda mrefu ambapo imekuwa ni vigumu kuweza kuyatunza. Hakuna yeyote mwenye busara na mtukufu mwenye shaka ya kwamba yanayoendelea katika baadhi ya miji ya Waislamu ni jarima baya na matendo yanayochukizwa yasiyokubaliwa na Dini, akili, mantiki na ubinaadamu. Pasina kujali jinsi kitendo kinavokisiwa ni haramu, jarima, tendo lenye kukemewa, ugaidi wa fedheha na ukhalifu wa khatari unaotaka kufungua njia ya shari itayoenea. Wao wameshikama vipi na maneno ya Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam):

”Hakika ya uhai wenu, mali zenu na heshima zenu juu yenu ni haramu kuvitumia vibaya.”

”Kitu cha kwanza watu watahesabiwa kwacho siku ya Qiyaamah ni uhai.”

”Muislamu hatoacha kuwa na uwezo wa kufanya matendo mazuri katika Dini yake midhali hamwagi damu ya haramu.”

”Allaah Anaonelea wepesi dunia nzima kutoweka kuliko kumuua mtu Muislamu.”?

Watu hawa wameshikamana vipi na ushahidiliaji ya kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah itapokuja siku ya Qiyaamah ili kugombana na wao? Imepokelewa katika as-Swahiyh kutoka kwa Usaamah (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

”Je, umemuua baada ya yeye kusema ya kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah?”

Akamkasirikia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka uso wake ukageuka kuwa mwekundu pindi alipomwambia Usaamah:

”Je, umemuua baada ya yeye kusema ya kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah?”

Usaamah akasema:

”Ee Mtume wa Allaah! Alisema hivo tu kwa sababu ya woga.”

Akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Je, uliufunua moyo wake? Ee Usaamah! Utafanya nini na ´nashuhudia ya kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah` itapokuja siku ya Qiyaamah ili kugombana na wewe?”

Usaamah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

”Nilitamani kuwa ni mtu ambaye sijasilimu kabla ya siku ile.”

Hivi ndivyo ulivokuwa ufahamu wa Maswahabah wachaji Allaah na Salaf wema juu ya damu iliyoharamishwa.

Kisha wanadai watu hawa wasiojulikana na waliosafishwa vichwa vyao eti wanasimamisha Shari´ah ya Allaah, wanasafisha kisiwa cha waarabu kutokana na washirikina na wanatangaza dola ya Kiislamu Iraaq na Syria. Tunamshtakia Allaah kwa watu wajeuri hawa vichwa vyao, umati wa watu waovu na vijana wapumbavu. Wanatenda kwa jeuri na kwa wehu ambapo wanasababisha fitina, khatari na maovu.

Hakika yanayoendelea katika baadhi ya miji ya Waislamu juu ya kumwagwa damu iliyoharamishwa, kuwauwa watu wasiokuwa na hatia, malipuaji, uharibifu, ufisadi na mengineyo ni jarima za haramu katika Shari´ah. Wana msingi wao katika fikira zilizopinda za Khawaarij na zinapingwa na Shari´ah, maumbile yaliyosalimika na akili ya sawa. Maadui wa Ummah wanawatumia ili kuuchafua Uislamu. Inatosheleza kwa utukufu wa Uislamu kuwa ni Dini ya ulaini, manufaa na ukuaji wa mji na sio Dini ya vurugu, uharibifu na malipuaji! Inatosheleza kwa utukufu wa sura ya Jihaad iliyowekwa katika Shari´ah, ambayo ndio ncha ya mkuki wa Uislamu, kupitia uharibifu huu, ufisadi na jarima! Ni manufaa gani watu hawa wameupa Ummah? Ni ushindi kiasi gani ambao watu hawa hawajawapa maadui wa Uislamu! Ni mara ngapi Dini na watu wa Dini, Da´wah na walinganizi, msaada na matendo ya kheri yamepatwa na madhara kwa sababu ya matendo haya machafu!

Ninawatahadharisha vijana wasiache wakadanganyika na mifumo ya watu hawa na wakawaamrisha kutorudi kwa wanachuoni Rabbaaniyyuun kuhusiana na mambo haya makubwa na kuwa wakati na kati. Kuweni hange kabisa na Fatwa zinazotoka kwa watu wasiojulikana wanaojiita Abu Fulani na Fulani na kujiunga na watu wenye maneno ya kupambia ya watu waliyosafishwa vichwa ya kidanganyifu.

Ni lazima kuchunga kila aina ya usalama na khaswa kila usalama wa ufikiriaji dhidi ya fikira zilizopinda na mielekeo potevu sawa ikiwa inahusiana na upetukaji mipaka, vurugu na Takfiyr au umagharibi, wanasekula na mengineyo. Ni hapa ndipo kunakuja ushirikiano wa familia, msikiti, shule na vyombo vya khabari mpaka watu waweze kusalimika na miji kuwa na amani.

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhahawiy adh-Dhwufayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/audio/9863
  • Imechapishwa: 19/04/2015