Wakati ilipojadiliwa kiasi ukhaliyfah Waislamu waliridhia utawala wa Seljuk[1] na ´Uthmaaniyyah. Waliridhia utawala wa kifalme kwa kujisalimisha na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Sikilizeni na tiini hata kama mtatawaliwa juu yenu na mtumwa.”

Ama kuhusu mtu ambaye anakuja katika nchi ambayo ina fujo na kuwaua watu ili yeye mwenyewe ajiite Khaliyfah, huyu ni Dajjaal katika mad-Dajjaal. Ninawatadharisheni kuzitia fahamu zenu kwake. Msitumbukie kwa wafuasi wake katika baadhi ya miji au kwa sababu ya vijisapoti alivyopata. Amewaua Waislamu wengi wa Ahl-us-Sunnah zaidi ya walivofanya baadhi ya makafiri. Zingatieni hili na tahadharini. Jambo hili ni khatari sana na Allaah ndiye Anajua zaidi.

————-

(1) Tazama http://en.wikipedia.org/wiki/Seljuk_Empire

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=145645
  • Imechapishwa: 19/04/2015