Khawaarij hawa walimfanyia uasi ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Wamekusanyika mahala kunakoitwa Haruuraa´ na baada ya hapo wakapewa jina la ”Haruuriyyah”. Utapata majina mengi ya Khawaarij; al-Qaaidah, ISIS… Kinachozingatiwa sio jina. Wote ni Khawaarij; Azaariqah, Haruuriyyah, Qa´dah ambao ni Khawaarij wabaya zaidi – wanachochea pasina wao wenye kufanya uasi. Na ni wengi walioje katika nchi yetu!

Wakati Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anhu) alipoona kichwa cha Khawaarij kimetundikwa kwenye mikuki Shaam akasema: ”Mijibwa ya Motoni.” Mtu aliekuwa pembezoni mwaka akasema: ”Unasema hivo?” Akasema: ”Hivi ndivo alivosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Mtu yule akasema: ”Hivi kweli ulimsikia akisema hivo?” Hivyo akasema: ”Ninaapa kwa Allaah la sivyo nitakuwa ni mtu mwenye ujasiri wa papara. Nilimsikia, nilimsikia, nilimsikia.” Baada ya hapo akamgeukia mtu yule na kumwambia: ”Ni wengi katika nchi yako.”

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba ni wengi katika nchi yetu. Allaah Afute shari yao na Awafichukue na Asiwafanye wakafikia malengo yao na wala Asiwape uongozi wowote. Ni njama za kidanganyifu ambazo zimeuchafua Uislamu na Waislamu. Pamoja na hivyo baadhi ya watu wanawasifu kama jinsi ´Imraan bin Hittwaan alivyomsifu aliemuua ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhu):

Ee mauwaji kutoka kwa mtu mtukufu kabisa

ambaye hakukusudia jengine zaidi ya radhi za Allaah

ninamfikiria na kuonelea kuwa

ni kiumbe aliye na mizani iliojaa mbele ya Allaah

Tazama sifa hizi za batili! Kwa hivyo msistaajabu kwa waliganizi wa batili kuwasifu watu hawa. Walinganizi wake na viongozi wao wanajulikana. Tunajua pia nchi ya Raafidhwah na viongozi wao. Kadhalika inatumika kwa Khawaarij. Tunasoma historia yao. Walioeneza fikira za Khawaarij zaidi leo ni kundi la al-Ikhwaan al-Muslimuun la kimisri lililoanzishwa na Hasan al-Bannaa. Halafu sumu ya Khawaarij ikaenezwa na Sayyid Qutwub. Kisha ikanywiwa na ´Abdullaah ´Azzaam na baada ya hapo ikachukuliwa na adh-Dhwawaahiriy na Usaamah bin Laadin. Watu hawa baadaye wakaieneza kwa wafuasi wao wote mpaka wakatiwa sumu kwa fikira hizi. Ukweli huu unatia uchungu kwa sababu tunaona jinsi watoto wote wanavowasifu watu hawa. Usistaajabu hilo likawa ni mlezi wao au mwalimu wao ndio anawasifu na kuwatukuza watu hawa.

al-Qaaidah, ambayo ni natija ya mapote na makundi haya, ndio jukwaa la leo. Kutoka kwenye al-Qaaidah ndio kumetoka ISIS na an-Nusrah. Hakuna tofauti kati ya an-Nusrah na ISIS. Ni kama sarafu moja yenye pande mbili. Tofauti yao ni ya kidunia na kisiasa. Adabu zao, fikira zao na ´Aqiydah yao ni moja. Ninashangazwa na wale wenye kuwakemea ISIS kwa ukali kabisa na kunyamazia an-Nusrah kana kwamba wao ndio wachaji Allaah na waliokaribu zaidi na Allaah. Hawa wote ni Khawaarij. Wana adabu moja, madhehebu moja na fikira moja hata kama watakuwa na tofauti.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Ramzaan al-Haajiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=147098
  • Imechapishwa: 19/04/2015