Swali: Sisi tuna kijana ambaye ni Salafiy ambaye ni dhaifu inapokuja katika kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah kwa kule kutangamana kwako na watu wenye utatizi. Kutokana na hilo baadhi ya Salafiyyuun wamesema kuwa sio Salafiy na wakati wengine wanasema kuwa ni Salafiy ambaye ni dhaifu inapokuja katika kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah. Bado anapata nasaha kwa kuzingatia ya kwamba watu hawa wenye utatizi bado wanakutana naye na wanamtembelea. Vipi tutataamiliana na kijana huyu?

Jibu: Salafiy ni lazima awe na mipaka ambayo hapaswi kuivuka. Kutokana na mpaka huo hakuna yeyote katika Ahl-ul-Bid´ah anayemsogelea. Wewe ni mtu unayefuata Sunnah. Utakapoanza kuwasikiliza watu wa Bid´ah na wapotevu utapotea au angalau kwa uchache kwenye njia ya kufanya hivo. Usiiweke nafsi yako khatarini. Usijijengee dhana nzuri juu ya nafsi yako. Hata kama utamsikiliza mtu wa Bid´ah anazungumza kwa kitu kisichokudhuru, mshairi anasema:

Usinywe sumu kwa kutegemea dawa

yamejaribiwa kwa matendo

Mtu wa Bid´ah ni kama sumu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mmiliki wa ngamia alie mgonjwa asiende kwa mmiliki wa ngamia alie na afya njema.”

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mkimbie mwenye ugonjwa wa ukoma kama jinsi unavyomkimbia simba.”

Fikira za ukoma ni khatari kuliko fikira za kimwili. Kuwa hange na Ahl-ul-Bid´ah. Kitendo cha kwamba yeye ni mtu wa Bid´ah na wewe ni Sunniy na unasema kuwa utamnasihi; kipi kinachosemwa? Mnakaa na kunywa kahawa, mnawasiliana kwenye Whatsapp, mnatembea pamoja kwenye gari moja na mfano wa hayo. Haitakikani kuwa kwa usulubu huo. Wewe ni Sunniy na huyu ni mtu wa Bid´ah. Ima atubu kwa Allaah au la sivyo acha kukaa naye. Usijizoweze kufanya matangamano na Ahl-ul-Bid´ah. Hii ni khatari:

Mwanamke chakavu hamnufaishi alie mzima

bali mwanamke mzima ndio atakuja kuchafuka

Tufaha iliooza ikiwa kwenye boksi moja na tufaha nzuri, tufaha zilizo nzuri pia zitaoza zilizoko karibu na zile zenye kuoza. Ukikaa karibu naye, atakuharibu. Ana haki ya nasaha tu. Baada ya hapo muache. Ni sawa kwa ndugu kumnasihi na ni sawa kuwa na mashaka naye katika mfumo wake. Hata hivyo inahitajia kupatikane ndugu watatu au wane wenye busara wakae naye na kumnasihi kwa njia nzuri kabisa na ya urafiki. Baada ya hapo ima awachague nyinyi au awachague Hizbiyyuun watu wa Bid´ah.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Yahyaa al-Bura´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=147098
  • Imechapishwa: 19/04/2015